Simba Queens Yachapwa, Yanga Yatakata

TIMU ya Simba Queens imedondosha pointi zote tatu kwa mara nyingine baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Baobab ya Dodoma, huku wapinzani wao Yanga Princess wakivuna alama tatu dhidi ya EverGreen.

Kocha wa Simba, Mussa Mgosi, ameliambia Spoti Ijumaa kuwa kujiamini kupita kiasi kwa wachezaji wake ndiyo kilichosababisha wapoteze mchezo huo, juzi huku lawama akizitupa kwa mwamuzi akidai kuchezesha mchezo huo chini ya kiwango.

Kwa upande wa Kocha wa Yanga, Hamis Kinonda, alisema ushindi waliopata utasaidia kuinua morali na moyo wa vijana wake ambao walionekana kukata tamaa kutokana na kupoteza mechi tatu mfululizo.
Huo unakuwa ushindi wao wa kwanza kwa Yanga baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo.
MaoniMaoni Yako