Mwanamke Ang'atwa na Nyoka Aliyekuwa ndani ya Sinki la Choo Wakati Akijisaidia!

'Nilihisi kama nimedungwa kisu kwenye mkalio ilikuwa uchungu sana'

Mwanamke mmoja nchini Australia "ameruka kutoka kwa kiti cha choo" baada ya kung'atwa na nyoka aina ya chatu.
''Nilihisi kama nimedungwa kisu kwenye mkalio ilikuwa uchungu sana, ghafla nilijipata nimeruka juu na kukimbilia nje nikiwa nusu uchi'' Richards aliviambia vyombo vya habari.
Bi Richards, 59, aling'atwa nyoka huyo katika nyumba ya jamaa zake mjini Brisbane mapema wiki hii.
Mtaalamu wa kushughulikia nyoka Jasmine Zeleny, aliyemtoa nyoka huyo kutoka chooni hapo amesema ni kawaida kwa nyoka kutafuta maji chooni hasa wakati wa msimu wa joto kali.
Zeleny amesema kuwa Bi Richards ametibiwa na kupewa dawa ya maumivu,akielezea kuwa aina hiyo ya chatu haina simu.
Mwanamke Ang'atwa na Nyoka Aliyekuwa ndani ya Sinki la Choo Wakati Akijisaidia!
"Njia ya nyoka huyo kutoka chooni ilizibwa wakati Helen alipokuwa akijisaidia, ndipo akamng'ata akihofia kudhuriwa," Bi Zeleny alisema
Chatu aina ya 'Carpet python' hupatikana sana katika pwani ya mashariki mwa Australia.
Huwa hana sumu lakini anapomng'ata mtu inapendekezwa adungwe sindano ya pepo punda.
Wiki za hivi karibuni Australia imekuwa ikishuhudia joto kali ambalo limevuja rekodi.
Wanyama wengi wa porini wameripotiwa kufa ikiwemo popo na samaki.
MaoniMaoni Yako