Monaco Imemtimua Meneja wake Thierry Henry Baada Ya Mechi 20.

Klabu hiyo inayoshiriki katika ligue 1 ilitangaza siku ya Alhamisi kwamba amesimamishwa kazi.

Mtangulizi wake Leonardo Jardim anatarajiwa kuchukua nafasi ya Henry, miezi mitatu baada ya yeye mwenyewe pia kufutwa kazi katika klabu hiyo.
Mabingwa hao wa Ufaransa wako katika hatua ya kushushwa daraja baada ya kupata ushindi wa mara tano chini ya uongozi wa Henry katika mashindano yote.
Meneja msaidizi, Franck Passi, alichanguliwa kama msaidizi wa Henry tarehe 20 mwezi Disemba , walipokuwa wakifanya mazoezi siku ya Ijumaa, klabu hiyo imesema.
Passi hapo awali alikuwa kama kocha wa muda wa klabu ya Marseille na Lille
Henry- aliajiriwa mwezi Oktoba - alikuwa ameomba msamaha kwa kumtusi beki wa Strasbourg Kenny Lala, katika mechi yaliyochapwa magoli 5-1 siku ya Jumamosi
Hapo awali alikuwa meneja msaidizi wa Ubelgiji.
Alikuwa ameorodheshwa katika orodha ya wanaowania kazi ya umeneja na klabu Aston Villa mwezi Oktoba kabla ya kuchukua nafasi ya umeneja na klabu ya Monaco.
Je, hatua hiyo ilitarajiwa?
Wadokezi katika klabu hiyo walikuwa wakiwaambia kila mmoja kwamba kazi yake iko salama. Usiku wa leo walitangaza kwamba atapigwa kalamu.
Ushindi wa mara mbili katika mechi 12 si dhihirisho kamili ya kazi njema. Alimtusi beki wa Strasbourg na pia kuwa na mabishano yalishuhudiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Labda uamuzi wake wa mwisho ulikuwa kuwaondoa baadhi ya wachezaji wanaocheza katika timu ya kwanza bila kuwaarifu wakuu katika klabu hiyo na hilo ndilo lililochangia kwa kufutwa kazi kwake.
Hivyo sivyo jinsi klabu hiyo ilivyotaka meneja huyo kuwa. Yote hayo yakiunganishwa ilimaanisha kwamba hangekuwa meneja tena.
Leonardo Jardim bado anaishi Monaco na hukutana na wachezaji wake barabarani akielekea katik duka la kuoka mikate . Yeye ndiye you katika nafasi nzuri ya kuvalia viatu vya Henry.Jardim alikuwa na matokeo bora kwa kushinda ligi mwaka 2017, kabla msimu huu ambapo mambo yalianza kuindea mrama timu hiyo.
MaoniMaoni Yako