Madam Ritha Afunguka Kuhusu Kumsaidia Pascal Kasiani

Madam Ritha Afunguka Kuhusu Kumsaidia Pascal Kasiani

Mwandaaji wa shindano la Bongo Star Search (BSS), Rita Paulsen amesema siyo lazima amsaidie Pascal Casian kwa sababu hawadaiani.Mwanamama huyo amesema hayo baada ya kuwapo kwa shinikizo mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari la kumtaka amsaidie matibabu Casian ambaye ni mshindi wa BSS mwaka 2009.

Casian ambaye kwa sasa ni msanii wa injili anaumwa kwa kipindi cha miezi minane sasa akiuguza majeraha ya ajali .
Katika ajali hiyo nyota huyo alipasuka kibofu cha mkojo, hivyo kuhitaji kiasi cha Sh25 milioni kwa ajili kwenda kutibiwa India.

Katika mahojiano maalumu na gazeti la MWANANCHI, Rita anasema amevumilia vya kutosha kusikia lawama na shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka amsaidie matibabu Casian. “Watu wanadhani ni lazima nimsaidie, kisa alipita kwenye shindano la BSS. Kimsingi Casian hanidai, nilishamalizana naye miaka tisa iliyopita,” anasema Rita.
MaoniMaoni Yako