Ijue Nguvu ya vazi la khanga Afrika Mashariki

Vazi la khanga au leso huvaliwa maeneo mbali mbali Afrika Mashariki na baadhi ya maeneo ya Afrika ya kati haswa katika maeneo ya pwani kama Dar es Salaam,Mombasa na Zanzibar.
Ijue Nguvu ya vazi la khanga Afrika Mashariki
Vazi hili likiwa asili yake ni Zanzibar, lilianzishwa kutokana na ushawishi wa wareno,ambapo khanga ya kwanza kuchapishwa ilikuwa khanga yenye rangi nyeusi na nyeupe,mwaka 1860,na jina la khanga hiyo ilijulikana kama khanga Zhamira na baadae vazi hilo likaendelea kukua katika ubunifu mbalimbali.
Jumuiya ya waandishi wa vitabu na wasanii wa "uchoraji na mashairi ,Jalada mobile literaly and Art wanazunguka katika miji nane ya nchi tano za Afrika mashariki,wakiaangalia historia na tamaduni ya kiafrika katika upande wa maandishi na ubunifu.
Wasanii hao wanaamini kuwa Khanga ina uhusiano mkubwa na Sanaa ,kutokana na maandishi yanayoandikwa kwenye khanga ,michoro na rangi zinazotumika .
Mwandishi wa BBC,Esther Namuhisa alijumuika nao katika mji wa Unguja katika tamasha la "kibao khanga" lililoandaliwa na Upendo women's Empowerment,The Khanga Book wakishirikiana na Jalada mobile.
Tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na wageni wapatao 100,lilijumuisha jumla ya mitindo 29,zilizoko sokoni zenye maneno yenye ujumbe mbalimbali kama wa mafumbo Mchungulia Bahari Si Msafiri',Upendo; Bahati Ni Kusafiri Na Wewe',Wawili wakipendana adui hana nafasi,
Licha ya kuibuka kwa nguo nyingine ambazo zinaweza kutumika kama khanga kwa mfano kikoi,mitandio na madira ,watumiaji wa Khanga wanadai kuwa bado khanga ina nafasi yake kubwa zaidi ya hizo zote kwa kuwa sasa wabunifu mbalimbali wa nguo wanatengeneza vitu kama;viatu,mikoba na mitindo mbalimbali ya nguo kutokana na khanga ,na kila mwanamke ana doti kadhaa za khanga nyumbani kwake na kuna maeneo ambayo .
Katika kisiwa cha Unguja ,Khanga inaelezwa kutumika katika hatua zote za maisha ya binadamu tangu anazaliwa mpaka anakufa.Mtoto anapozaliwa huwa anavalishwa khanga,akiwa katika hatua ya kuingia ujana;wasichana kwa wanaume huvaa khanga na kwenye mazishi khanga ufunika mwili wa marehemu.
Vilevile , Khanga inaaminika kuwa ni vazi la siri pia kwa kuwa linahusisha mahusiano ya mapenzi ndio maana wanaume huwa hawawezi kuvaa vazi hilo hadharani.
Pamoja na umaarufu mkubwa wa vazi hilo kutumika katika ukanda wa pwani ,Khanga inachapishwa katika nchi za bara la asia kama India na China , wabunifu na waandishi wa khanga hizo bado wana changamoto ya kupata faida katika ushiriki wao wa ubunifu ,kwa mfano wanawake wengi ndio wanatuma maandishi ya khanga hizo ila malipo ni doti moja ya khanga.
MaoniMaoni Yako