Diamond Ampa SIFA Kedekede Tanasha


Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amempa sia za kutosha mpenzi wake mpya kwa kudai kuwa mwanamke anatakiwa awe anafanya vitu vyote kama Ronaldo.

Diamond amesema kuwa sababu za kunenepa kwake ni mapishi ya mpenzi wake yanachangia na hata style ya nywele mama yake na mpenzi wake huyo wamechangia.

"Mapishi shemeji yenu anapika sana, matunzo moyo umetulia, napendwa nadekezwa natengenezwa style za nywele Baby nyoa hivi, mwanamke inatakiwa awe anafanya vitu vyote awe kama Christino Ronaldo," amesema Diamond Dizzim Online.
Hata hivyo, Diamond amesema kuwa anampenda sana msichana huyo kwasababu ni mtu ambaye hana makuu, mstaarabu hana majigambo.

MaoniMaoni Yako