Thursday, January 24, 2019

Dalili za MUME Anayetembea Kimapenzi na MSICHANA wa Kazi za Ndani "HAUSIGELI"

Tags

Dalili za MUME Anayetembea Kimapenzi na MSICHANA wa Kazi za Ndani "HAUSIGELI"

DALILI YA KWANZA
Ishara ya kwanza ya mwanaume ambaye tayari yupo ndani ya uhusiano wa kimapenzi na msichana wa kazi ni kupenda sababu za kumwamsha mfanyakazi huyo  hata pale anaporudi na kumkuta amelala.

Utakuta baba amerudi nyumbani usiku wa saa sita, mkewe anamfungulia mlango, akishaingia na kukaa, anaanza:
“Dada amelala?”
Mke: “Ndiyo.”
Baba: “Mwamshe nimpe kazi f’lani.”
Mke unaweza ukamtetea sana msichana, lakini mumeo akasimamia msimamo ule ule.


Sasa utakapomwamsha, akifika, mumeo utamuona anavyojipinduapindua.
“Hii mboga umepika wewe dada?”
“Hapana, mama.”

“Ooo. Ulifua zile soksi zangu?”
“Ndiyo baba.”
“Sawa kalale.”
Mke unajiuliza, sasa kumwamsha kote kule ndiyo maswali yenyewe hayo tu.
Sasa tuendelee…

Katika hali kama hii, wewe mke jaribu kuwa makini sana. Hakikisha hutoi nafasi kwa mumeo kumfikia au kuwasiliana na hausigeli kwa kitu chochote. Kama ni maji ya kuoga tenga wewe, vitu ambavyo vinawezekana kufanywa na wewe vitimize ili kuukata uhusiano hata kama utakuwa hujathibitisha kama upo!

Tatizo kubwa ni kwamba, wanawake wengi siku hizi wanawafanya wasichana wa kazi ndiyo wenye nyumba, wao wasaidizi, wakati zamani, hausigeli ndiye msaidizi wa kazi za ndani, mambo mengine yote ni kwa akina mama wenyewe.

DALILI YA PILI
Ishara hii inatakiwa mke mwenye utambuzi sana, yaani awe na ufahamu wa hali ya juu vinginevyo anaweza kukurupuka na kumbwatukia mumewe kumbe hana  habari na msichana wa kazi.

Ila kwa wale ambao wana uhusiano sasa, ukimwona mumeo ana tabia ya kuchelewa kulala eti yupo sebuleni, mke changamka, hapo pana jambo.
Mume anayefanya hivyo hutoa nafasi kwa mkewe kwenda kulala na yeye kunyatia chumbani kwa hausigeli kuduu naye.

Sasa endapo mke utakwenda sebuleni na kumkuta mumeo anajifanya kukodolea macho tivii ili ujue anaangalia vipindi, jaribu na wewe kuchunguza aina ya kipindi, ukikuta ni taarifa ya habari ya Sky News,CCTV, CNN, BBC au Al Jazeera, ujue huyo mwongo tu, hana lolote.
Lakini usiishie hapo, jifanye na wewe unakaa pembeni yake kuangalia taarifa hiyo  ya habari. Utamuona yeye anasimama na kusema…

“Tukalale mke wangu.”
Kama wakati wa kwenda kulala wewe utatangulia, yeye lazima aingie chooni kwanza, anajifanya anajisaidia haja ndogo lakini anachotaka ni wewe uingie chumbani, yeye aingie kwa hausigeli ili ampige busu japo moja tu, maana anajua dili limeshatibuka.
Lakini dalili hii ni kwa mume ambaye hapo nyuma hakuwa na tabia ya kukaa sebuleni peke yake na kuangalia tivii.

Kwa upande wa hausigeli aliye katika uhusiano na baba mwenye nyumba, huwa hivi…
Wakati baba amekaa sebuleni usiku akiangalia tivii ‘kiuongo’, yeye anaosha vyombo nje, tena si ajabu amevitawanya kiasi kwamba, kama ni kumaliza ataweza kwenda hasi usiku wa manane.

Na kila baada ya dakika tano, msichana huyo ataingia ndani na kupita mbele ya baba. Lengo lake ni kusoma mazingira kama mama mwenye nyumba amelala.

Kwa vile wao si waanzaji (kama ilivyo tabia ya mwanamke), basi unaweza kumwona anashikashika vitu vya sebuleni, kama vile kuweka sawa vitambaa vya makochi (japo ni usiku), kufuta meza, kabati au wakati mwingine kupanga CD za muziki au filamu ambazo zipo kwenye shelfu lake. Mambo hayo anayafanya huku vyombo vikimsubiri nje!

Hapo anachotaka, baba amuone kirahisi na kuanza kumtekenya-tekenya, kumshika-shika hatimaye ‘kumalizana’.

Utashangaa, ukifuatilia sana, utakuta hausigeli akishamalizana na mume, vyombo anaviingiza ndani na kuvimalizia kesho yake asubuhi.
Kwa maana hiyo pia, wake za watu wawe macho na wasichana wa kazi wanaoshindwa kumaliza kuosha vyombo usiku.

MAENEO YA UFUSKA
ni vyema niweke wazi maeneo ambayo ma-baba wenye nyumba ndiyo hupenda kutumia kufanya mapenzi na wasichana wa kazi.
Ni vigumu sana kukuta wawili hao wanamalizana sebuleni (ingawa inawezekana sana) kwani ni eneo hatari kuliko yote ndani ya nyumba.

Uchunguzi wa kina wa kimazingira umegundua kuwa, kati ya maeneo hatari kwa fumanizi ndani ya nyumba ni sebuleni.
Wengi waliowahi kufumaniwa, mfano mume kula uroda na shemeji yake (mdogo wa mkewe) au binti kuliwa uroda na hausiboi, ilikuwa sebuleni.

Aidha, sebuleni ndiyo mahali panapofikwa kwa mara ya kwanza na watu waliolala ndani ya nyumba kuliko sehemu nyingine yoyote.
Kwa hiyo, mababa wengi sasa hukwepa sebule na kwenda chumbani kwa msichana, stoo, bafuni, jikoni kama liko pembeni na uani, hasa maeneo yenye vificho kama nyuma ya karo au kama kuna sehemu kumesimamishwa vitu chakavu.

Chooni si sana kwa sababu ni eneo linalofikwa na watu kila wakati karibu usiku kucha.
Sasa hatari ipo hivi, mke asiyejua haya, kama mumewe ataendelea kimapenzi na hausigeli, hufikia wakati uhama nyumba. Namaanisha kwamba, hufika mahali wakitaka kukutana kimwili, wanakwenda gesti.

Gesti zao mara nyingi ni nyuma ya nyumba au mtaa wa pili, huwa hawaendi mbali sana kwa kuogopa muda wa msichana kufanya kazi za ndani.  
Tutaendelea wiki ijayo. jamani, tuone dalili ya tatu.