Wema Sepetu na Hamisa Hapatoshi, Ugumba wa Wema Vs Uchawi wa Hamisa, Baba Diamond Aingilia Kati

Wema Sepetu na Hamisa Hapatoshi, Ugumba wa Wema Vs Uchawi wa Hamisa, Baba Diamond Aingilia Kati

VITA imekolea! Ni kati ya mwanadada Wema Isaac Sepetu na mwanamama Hamisa Hassan Mobeto ambapo hapatoshi kiasi cha baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’ kuingilia kati, Risasi Mchanganyiko limeelezwa. Wema na Mobeto, wote walishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond ambapo Mobeto alijaliwa kupata naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Abdul Nasibu ‘Dylan’. Timu mbili, moja ikiwa ni ya Wema almaarufu Team Wema na ile ya Mobeto yaani Team Hamisa zimekuwa zikishambuliana tangu lilipoibuka sakata la Mobeto kuhusishwa na uchawi.UCHAWI VS UGUMBA

Wakati Mobeto akihusishwa na kushambuliwa kwa ishu ya uchawi, Wema yeye anashambuliwa kwa ishu ya ugumba au kutopata mtoto.

Mara baada ya kuvuja kwa sauti iliyodaiwa ni ya Mobeto akizungumza na mganga amsaidie ili apendwe na kuolewa na Diamond, Wema alidaiwa kuingilia sakata hilo na kuwa upande wa familia ya Diamond kushiriki ‘kumnyuka’ Mobeto kwa maneno. “Allah atunusuru na husda bin hasadi, maana akina binti mchawi hawakawii wakatafuta hata wenye vitochi…” aliandika Wema akimjibu mmoja wa mashabiki wake juu ya sakata hilo.WEMA NA MAMA D

Wema anadaiwa kuungana na mama Diamond, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na dada wa jamaa huyo, Esma Khan ambao ndiyo hasa waliodaiwa kuvujisha sauti hizo walizodai kutumiwa na mganga huyo. Baadaye Diamond alipofunguka juu ya Mobeto kumloga, pia Wema alidaiwa kumuunga mkono Diamond na kupeleka mashambulizi ya mafumbo kwa Mobeto.

NANI KIPENZI CHA WATANZANIA?

Kama hiyo haitoshi, vita hiyo ilikolezwa na nani anastahili kuwa Tanzania Sweetheart (Kipenzi cha Watanzania) na Dada wa Taifa kati ya Wema na Mobeto ambapo jambo hilo limeendelea kusababisha tafrani mitandaoni. Katika ishu hiyo, Team Wema ndiyo walioanza kumwita Wema jina hilo la Tanzania Sweetheart kabla ya hivi karibuni ambapo Team Hamisa nayo ilianza kumwita Mobeto jina hilo.MOBETO ALAMBA MADILI

Mbali na kumwita Mobeto jina hilo, lakini wamekuwa wakidai ndiye habari ya mjini kufuatia kulamba madili mbalimbali ndani ya muda mfupi kama kuwa balozi wa nywele, kuwa mmoja wa ma-MC wa Shindano la Miss Tanzania 2018 na dili lingine nchini Marekani ndani ya muda mfupi wakati Wema hana chochote.

TUKUTANE MLIMANI CITY

Kwa upande wake Team Wema imekuwa ikitamba kwamba dawa ya Mobeto ipo jikoni na watamkomesha Septemba 28, mwaka huu, siku ya kuzaliwa Wema ambapo kutakuwa na shughuli baab’kubwa itakayokwenda sambamba na uzinduzi wa filamu yake ya Day After Death (D.A.D) akiwa na staa wa sinema wa Ghana, Van Vicker kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.BABA D AINGILIA KATI

Baada ya kimbembe hicho kuzidi kushika kasi kila kukicha, baba mzazi wa Diamond aliamua kuingilia kati ambapo alionekana kumkingia kifua Mobeto huku ikifahamika kuwa huwa anampenda pia Wema. Akizungumza na gazeti hili juu ya chanzo cha yote ambacho ni uchawi, Baba Diamond alidai kuwa siyo ishu kwa Mobeto kuambiwa anamloga Diamond kwani wapo watu wengi ambao wamekuwa wakimzushia kulogwa. Alisema anashangaa kuhusiana na taarifa zinazotapakaa kwenye mitandao na sehemu mbalimbali kuwa Mabeto anasadikiwa kumloga Diamond ambaye ni mzazi mwenzake.“Ukiwa siyo mtu wa bahati, kweli hubahatiki. Katika ishu hii jumba bovu limemwangukia tu Mobeto. “Kuhusiana na suala la Diamond kulogwa na Mobeto, si kweli. Diamond analogwa na watu kibao, lakini kwa hili la sasa, ninashangaa ameonekana Mobeto tu,” alisema baba D na kuongeza:“Diamond analogwa na wasanii wenzake na siyo Mobeto, analogwa na wanawake wengi, analogwa na watu wanaojidai ni Team Diamond. “Wanawake wanaomloga Diamond ni wale wanaotaka kuwa naye karibu. Tuache kumsingizia Mobeto, ukweli ni kwamba Diamond analogwa na watu wengi tu wakiwemo wasanii anaoshindana nao kimuziki.
KUHUSU WEMA NA MOBETO

“Kuhusu Mobeto na Wema mimi ninawashauri wakae chini, wapatane na wawe marafiki kama zamani ili maisha yasonge. “Zaidi ninamshauri Mobeto kuwa mvumilivu na kuamini mambo haya yatapita na mimi ninampenda sana Mobeto.”BABA D KAMA KAWAIDA

Mara kadhaa baba Diamond amekuwa akitofautiana na ‘memba’ wengine wa familia ya Diamond kama ilivyotokea kwenye sakata hili ambapo ndiye pekee yupo upande wa utetezi wa Mobeto kama alivyowahi kufanya kwa Wema kipindi kile anatengana na Diamond.

STORI: Zaina Malogo, Risasi Mchanganyiko.