Wema Sepetu Aja na Ujio Mpya!

Malkia wa filamu Wema Sepetu aka Tz sweetheart ametangaza ujio wake mpya baada ya ukimya wa muda mrefu.

Mrembo huyo atafanya matukio mawili kwa pamoja, uzinduzi wa filamu yake mpya ‘Dad’ alioshirikiana na Van Vicker kutoka Nigeria pamoja na kusherekea birthday yake ambayo ameiita Bithday Gala.
“The Moment tuliokuwa tukisubiria saaaaanaaa sio,  I hope you are Ready, aliandika Wema Sepetu kupitia picha ya matangazo ya show hiyo.
Hili litakuwa ni tukio la kwanza la mrembo huyo toka ahukumiwe na Mahakama ya Kisutu baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Wengi wanadai umaarufu wa Wema umeshuka tofauti na kipindi cha nyumba ambacho inadaiwa alionekana kukubalika zaidi

SOMA NA HII: NAFASI ZA AJIRA ➤

Job Opportunity at Fast Link, Reservation Sales Agent

Job Opportunity at Fast Link, Reservation Sales Agent


MaoniMaoni Yako