Monday, September 10, 2018

UWOYA AFUNGUKIA KUWA NA BWANA DUBAI

Tags


WATU wengi wanajua ubuyu wenye ladha ni ule mwekundu tu, lakini siyo kweli kwani kuna ubuyu mwingine mweupe, blu na hata kijani na yote ina ladha moja! Ubuyu uliotua mezani kwetu wiki hii unadai kwamba staa mwenye mvuto wa kipekee Bongo Muvi, Irene Uwoya, juzikati alikuwa anatanua huko Dubai na mwanaume mwingine tofauti na mumewe ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’. Chanzo chetu kilichomwaga ubuyu huo kilidai kuwa, Uwoya na Dogo Janja hawana maelewano tena ndani ya ndoa yao hivyo mwanamama huyo alikwenda kupumzisha akili yake huko

Huku ikidaiwa ameambatana na mwanaume huyo mwingine. “Uwoya ameona kama haelewi kabisa kuhusiana na ndoa yake na ni kama haipo kabisa ndiyo maana aliamua kuondoka kwenda kutuliza akili nje ya nchi. “Lakini ilidaiwa huko alikwenda na mtu mwingine mwenye pesa zake nyingi tu,” alisema mtoa ubuyu wetu.