Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 10.09.2018: De Jong, Shaw, Pogba, Ramos, Salah, Herrera, Defoe, Lemina

Ofa za Tottenham na Barcelona zimekataliwa kwa kiungo wa kati wa Ajax mwenye miaka 21 Frenkie de Jong. (Mundo Deportivo - in Spanish).

Beki wa Manchester United wa miaka 23 raia wa England Luke Shaw anasababisha klabu yake kungoja kuhusu mkataba wake mpya, Mkataba wake wa sasa unakamilika mwishoni wa msimu.
Kiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Paul Pogba 25, anasema kumekuwa na vitu vidogo kati yake na Jose Mourinho lakini uhusiano wao ni ule ule. (TF1, via Express)
Gareth Southgate atafanya mabadiliko tisa kwa kikosi chake cha England kwa mechi ya siku ya Jumanne na Uswizi. (Mirror)
Vilabu vya ligi ya Premio vitakubaliana kuhusu tarehe ya misho ya kununua wachezaji iwe Agosti 31. (Sun)
Kiungo wa kati wa Real Madrid mwenye miaka 32 Sergio Ramos anasema alipokea vitisho vya kuuawa kufuatia kuhusika kwake wa jeraha la mshambulizi wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah, 26, wakati wa fainali ya ligi ya mabingwa mwezi Mei. (ESPN)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema anata kurudi kwenye usimamizi hivi karibuni. (RTVE, via Marca)
Roma wanataka kumsani kiungo wa kati wa Porto mwenye miaka 28 Hector Herrera. (Corriere dello Sport - in Italian)
Mshambuliaji mwenue miaka 35 wa Bournemouth Jermain Defoe anatathmini taaluma katika usimamizi. (Bournemouth Echo)
Kiungo wa kati wa Southampton 25 mzaliwa wa Gabon Mario Lemina, fainia yake ya kuendesha gari kwa kasi imepunguzwa kutoka pauni 96,425 hadi pauni 2,000 kwa sababu alihukumiwa nchini ya sheria isiyosahihi. (Southern Daily Echo)