Sipendi na Nimechoka haya Makalio Makubwa!.. Aeleza kwa Uchungu Mrembo Kim Kardashian

Mwanamitindo Kim Kardashian  ameushangaza ulimwengu baada ya kudai kuwa hapendi kabisa muonekano wake wa sasa unaomuonesha ana makalio makubwa kiasi kwamba analia kila siku yapungue.
Akiongea kwenye episode ya  Keeping Up With the Kardashians ya Jumapili illiyopita, dada yake Kourtney alitoa maoni yake kuwa kwa sasa Kim anaonekana makalio yake yameongezeka ukubwa “Kim, naona kwa sasa kila picha unayopiga ukiwa umekaa unaonekana makalio yako yameongezeka ukubwa!,” alihoji Kourtney.
Hata hivyo, mama yao Kristen alionekana kukerwa na maoni hayo ambapo alimwambia  Kourtney kuwa amekosea kwa kumtolea kauli hiyo kwani Kim mwenyewe anapenda kuwa na muonekano huo wa makalio makubwa.
“Najua anapenda kuwa na makalio makubwa na mimi sijafanya kosa lolote kumwambia hivyo,“amejibu Kourtney huku akimuangalia mama yake na kisha wote kuangua vicheko.
Baada ya sekunde kadhaa Kim Kardashian alitoa jibu ambalo liliishangaza familia yote, ambapo alisema kuwa anachukizwa na ukubwa wa makalio yake, jambo ambalo linamfanya alie kila siku namna ya kuyapunguza.
“Niwe muwazi sipendi kabisa kuwa na makalio makubwa, nalia kila siku kuyapunguza,ameeleza Kim huku akiwa na uso wenye hasira juu ya umbo lake la sasa.
Mwaka 2010, Kim alipatwa na skendo kuwa alifanyiwa upasuaji mdogo ili kuongeza makalio yake. Jambo ambalo lilizua gumzo mtandao lakini mwenyewe hajawahi kujitokeza wazi kuthibitisha taarifa hizo.