Wednesday, September 12, 2018

Rosa Ree Afunguka Kuhusu Kolabo na DC Jokate Mwegelo

Tags

Msanii wa muziki Bongo, Rosa Ree amesema picha iliyowahi kutoka kati yake na DC wa Kisarawe kwa sasa, Jokate Mwegelo haikuwa kwa ajili ya wimbo.

Rapper huyo kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema picha hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya project ya nywele waliyotaka kuifanya kwa pande zote mbili.

"Actual ilikuwa si ngoma tulikuwa tunafanya project nakumbuka nilikuwa The Industry, tulikuwa tunafanya project ya nywele, kwa hiyo tulikuwa tunafanya kuweka brand ya Rosa Ree na Kidoti pamoja, so was it, yeah!," amesema.

Rosa Ree kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la One Way.