Wednesday, September 12, 2018

Petit afunguka kuhusu kuchepuka na kumpachika Mnyarwanda mimba

Tags

Baada ya mwanadada maarufu mtandaoni, Mange Kimambi kuvujisha sauti zinazodaiwa kuwa za Petit Man akisikika akizungumza na mwanadada anayedaiwa kuwa mpenzi wake Mnyarwanda, mume huyo wa Esma mdogo wake Diamond, amefunguka.

Akiongea na U Heard, Petit alidai yeye anashinda na watoto kwahiyo kama kuna mwanamke ambaye anadai anamtoto wake basi ajitokeze.

“Azae tu sisi hatukataagi watoto,” alisema Petit baada ya kuambiwa kuna mwanamke Mnyarwanda ana mimba yake.

Aliongeza,”Watoto kwangu ni baraka kweli kweli, kwa sasa nina mtoto mmoja tu, nahitaji waongezeke familia iwe kubwa zaidi, kwahiyo yeye kama ana kibendi changu azae huu sio muda wa maneno,”

Mapema leo asubuhi Mange alikuwa kwenye malumbano na mke wa Petit, Esma na ndipo mwanadada huyo ambaye anaishi Marekani akaamua kuvujisha sauti hizo ambazo anasikika Petit akimbembeleza Mnyarwanda huyo.