Mourinho aambiwa amtumie vipi Rashford

 GWIJI wa Manchester United, Gary Neville amemwambia Jose Mourinho namna nzuri ya kumtumia Marcus Rashford ni kumchezesha nafasi ya mshambuliaji wa kati.
Neville, aliyewahi kuwa nahodha wa Man United amesema Rashforda atumike kwenye nafasi moja kwa muda mrefu na si kumhangaisha kama anavyofanya Mourinho kwa sasa.
Gwiji huyo amesema, Mourinho amekuwa akimtumia mshambuliaji huyo mara pembeni, kati na wakati mwingine kwenye benchi.
Amesema, anachoamini Mourinho ni kwamba mshambuliaji wake wa kati ni Romelu Lukaku tu, lakini Neville alisema anaweza kumtumia sambamba na Rashford kwenye nafasi hiyo na Man United itavuna matokeo mazuri.
“Marcus Rashford, hana shida ni mchezaji kijana, hivyo suala la kubadilishwa nafasi, leo hapa kesho kule haliwezi kumsumbua, lakini ingependeza zaidi kama angetumika kama mshambuliaji wa kati, si hii mara kulia, mara kushoto, mara kati, mara anatokea benchi, inampa ugumu," alisema.

Nafasi za kazi mpya zilizotangazwa leo Jumatano 12 September 2018- Apply Now