Miriam Odemba AmemvaaDiamond Kisa Hamisa Mobetto

Miriam Odemba AmemvaaDiamond Kisa Hamisa Mobetto
MWANAMITINDO aliyewahi kutamba miaka ya 2000, Miriam Odemba amemvaa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kumpa vipande vyake kuwa, hakustahili kumsema vibaya mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa kumrushia tuhuma nzito ambazo zimemfanya adhalilike.  Akizungumza na Risasi Jumamosi akiwa nchini Ufaransa, Odemba alisema kuwa hakuna kitu kibaya kama kumtolea maneno ya kashfa mzazi mwenzio na hata kama kuna sehemu aliteleza, busara inatakiwa kutumika.

“Yaani mimi sijapendezwa kabisa na alivyofanya Diamond, kwa maana anapaswa kuheshimu hata kile kiumbe kilichowaunganisha. Kama kuna matatizo ya kifamilia ni vyema kukaa chini na kumalizana, lakini siyo kuyaweka kwenye kadamnasi kama alivyofanya Diamond. Kuna siku watakutana kama wazazi, hivi atajisikiaje? Amekosea sana,” alisema Odemba ambaye kwa sasa yupo nchini Ufaransa akiendelea kufanya shughuli zake za mitindo