Mastaa Wakali wa Holywood Wasiopenda Kuoga au Kufanya Usafi wa Mwili wao

Johnny Depp na Vanessa Paradis
Mwigizaji  Johnny Depp na mpenzi na mwimbaji wake wa zamani, Vanessa Paradis, wanasemekana hawapendi kuoga.  “John huwa ananuka kwani huoga mara chache sana,” kinasema chanzo kimoja cha  Fox News  na kuongeza kwamba na Vanessa yake yuko  hivyohivyo,  na kwamba walikuwa wamekutana watu wasiopenda afya zao.

Robert Pattinson
Mwanamuziki, mwanamitindo na mwigizaji huyo hivi sasa ni msafi kidogo ambapo anasemekana hapo nyuma alikuwa ananuka vibaya. Alipoulizwa na shirika la habari la Extra iwapo kweli alikuwa hajaweka mafuta kwenye nywele zake kwa majuma kadhaa, alijibu kwamba hajui. Akaongeza:  “Sioni maana ya kusafisha nywele.  Sioni pia haja ya kusafisha nyumba yangu; sijali.”

Zac Efron
Mwigizaji huyo si mpenzi wa kuoga pamoja na kwamba huwa anacheza mpira wa kikapu.  “Zac si shabiki wa kuoga, akimaliza kucheza huendelea na maisha bila kwenda bafuni,” kinasema chanzo.

  ➤:AJIRA MPYA BOFYA LINKI HII:
Leonardo DiCaprio
Mwigizaji na prodyuza wa filamu, Leonardo DiCaprio, anasemekana anapenda sana mazingira kiasi kwamba hataki maji yatumike ovyo kwani yanasaidia kuotesha mazingira.  Yeye huoga mara chache kwa siku na hapendi manukato akisema hayana uasili wowote.  Kutokana na kuwa katika hali hiyo, nyumba yake na yeye mwenyewe hutoa harufu mbaya.

Cameron Diaz,
Mwigizaji  Cameron Diaz, hapendi kutumia pafyumu akisema zinanuka, hasa zikipuliziwa kwenye kwapa zisizonyolewa.  Diazi anasema hajatumia pafyumu kwa karibu miaka 20 kwa vile hunuka vibaya.  Anasema: “Dawa ni kunyoa makwapa ili kuondoa harufu ambayo hubakizwa humo na pafyumu.”

Julia Roberts
Mwigizaji huyo pia anasemekana huwa ananuka.  Kisa?  Hapendi kutumia pafyumu kwa vile anasema hicho si kitu anachokipenda.  Inasemekana pia Julia hapendi kabisa kuoga kila mara, anaweza kukaa siku kadhaa bila kuoga.  Badala yake anapenda maji yatunzwe kwa ajili ya mazingira.  Isitoshe, anapenda kusikia harufu yake ya mwili yenye mafuta ya asili na hapendi kuziosha nywele zake kila mara kwani ni ngumu mno.

MaoniMaoni Yako