Mapya Yaibuka Kuhusu Djuma Juu ya Safari ya Mtwara


Wakati kikosi cha Simba kikiratajiwa kuondoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea Mtwara, taarifa za kidukuzi zinaeleza kuwa Kocha wake Msaidizi, Masoud Djuma atasalia Dar es Salaam.

Kocha huyo ambaye aliteka vyombo vya habari wiki kadhaa zilizopita kwa kuripotiwa kuwa ataondoka Msimbazi, inaelezwa ataikosa safari hiyo.

Inaelezwa kuwa Djuma atasalia jijini Dar ili kikonoa kikosi cha pili kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Kikosi cha Simba kinaelekea leo Mtwara na Ndege kikiwa na jumla ya wachezaji 20 sambamba na Kocha wake Mkuu Patrick Aussems, bila ya Meneja wa timu, Richard Robert.

Robert ataikosa safari hiyo baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa muda wa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka.

Simba inaelekea Mtwara kukabiliana na Ndanda ikiwa na rekodi ya kutokufungwa na timu hiyo tangu ipande daraja mwaka 2014.