Lulu Michael Kavunja Ukimya Kwa Kumwandikia Maneno Matamu Mpenzi Wake


Baada ya kimya cha muda mrefu cha takribani siku 324 mitandaoni, hatimaye Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael almaarufu Lulu amerudi rasmi kwa kumuandikia ujumbe mahsusi mpenzi wake Majizzo ambaye pia ni Mkurugenzi wa EFM na TV-E .

Lulu ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika; Lover,Best Friend,Business Partner,Ride Or Die And A Shoulder To Always Cry On...!! .

Asante Kwa Kunionyesha Maana Halisi Ya Upendo Wa Agape(KIUNGU)❤️❤️❤️
Baraka Zikufuate Siku Zote Za Maisha Yako.

Happy Birthday Baba G....I Love You💕💕💕
@majizzo @majizzo

Lulu hajawahi kuposti kitu chochote kile mtandaoni tangu mwaka jana ahukumiwe jela na baadae kutolewa jela kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ujumbe huo pia ameutoa leo ikiwa ni siku ya kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa Majizzo. Mashabiki wake wameoneshwa kufurahishwa zaidi na kitendo hicho