Saturday, September 15, 2018

Kayumba Aingilia Penzi la Irene Uwoya, Dogo Janja Afunguka Anavyopendwa na Irene Uwoya

Tags

Kayumba Aingilia Penzi la Irene Uwoya, Dogo Janja  Afunguka Anavyopendwa na Irene Uwoya
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Kayumba amefunguka na kujigamba kuwa anapendwa na muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya ambaye ni mke halali wa mwanamuziki Dogo Janja kutokana na kazi zake anazozifanya.

Kayumba amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE kutoka EATV, kwa njia ya simu mara baada ya wawili hao kuonekana katika kumbi za starehe majira ya usiku wakila raha bila ya kuwa na wasiwasi wa jambo lolote huku wengine wakidai Kayumba anatoka kimahusiano na mrembo huyo.

"Irene Uwoya ni mshkaji wangu sana pia anapenda kazi zangu lakini sidhani kama Dogo Janja anafahamu urafiki wetu huu tuliyokuwa nao, huwa tunakutana na mara nyingi na kupiga stori tu. Kikubwa anachoniambia Uwoya kuwa ananipenda kutokana na muziki wangu na jinsi ninavyoimba. Vitu vingine siwezi kuzungumza kwasababu yamekaa kibinafsi sana ila mimi ninachokijua ni kuwa anapenda muziki wangu tu basi", amesema Kayumba.

Mwanamuziki Kayumba.

Mbali na hilo, Kayumba kupitia ukurasa wake wa kijamii usiku wa kuamkia leo ameweka kipande cha 'video clip', kinachomuonesha Irene Uwoya akiimba wimbo wa 'mazoea' ambao uliotolewa na msanii huyo miezi mitano iliyopita na kuzua maswali mengi kwa mashabiki zake juu ya video hiyo.