Wednesday, September 12, 2018

Juuko, Niyonzima wapewa masharti Simba

Tags


Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba, Juuko Murshid raia wa Uganda na Mnyarwanda Haruna
Niyonzima, wamerudishwa kwenye timu lakini kwa makubaliano maalumu.
Wachezaji hao ambao wako jijini Dar es Salaam, walikaa kikao 'kizito' na Kaimu Rais
wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' na kufanya makubaliano hayo.
Wachezaji hao ambao hawakuwa pamoja na timu kwa kipindi kirefu kutokana na madai ya
utovu wa nidhamu. Sehemu ya masharti yao ni kwenda sawa na matakwa ya klabu.
Wachezaji hao hawajaanza mazoezi ya pamoja na wenzao na wanatarajiwa rasmi kesho
Alhamisi ambapo watafanya pamoja na kikosi cha pili ambacho kitabaki jijini Dar es
Salaam na kocha msaidizi, Mrundi Masoud Djuma.
Baadhi ya wachezaji ambao ni 20, pamoja na benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu,
Patrick Aussems isipokuwa Djuma, wataondoka kesho kwa usafiri wa ndege kwenda