Thursday, September 13, 2018

Johari Awekewa 'Madawa ya Kulevya baa'

Tags

STAA wa muda mrefu katika tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ hivi karibuni yamemkuta mazito akiwa baa baada ya watu wasiojulikana kumuwekea vitu vilivyodaiwa ni madawa ya kulevya kisha kumuibia kila kitu.

Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina kilitutonya kuwa, siku ya tukio Johari alifika katika baa hiyo iliyopo maeneo ya Sinza jijini Dar na kuanza kupata kinywaji akionekana kama aliyekuwa akimsubiria mtu.

“Akiwa anaendelea kupata kinywaji, kuna watu walikuja wakakaa pembeni yake, mimi sikuwajua ni akina nani. Kuna wakati Johari alienda chooni, aliporudi sikujua kilichoendelea ila nilishangaa kumuona kama amesinzia hivi na wale watu wa pembeni yake sijawaona.

“Baadaye mwenyewe alipozinduka alijikuta hana pochi. Alichanganyikiwa na pombe yote ilimuishia, sisi tulihisi aliwekewa madawa ya kulevya na ndipo akafanyiwa mchezo huo,” alitiririka sosi huyo.

SOMA NA HII👉NAFASI ZA KAZI 25 KUTOKA AMREF HEALTH AFRICA - Semptember 2018 - APPLY NOW! - Ajira Tanzania

Katika kupata undani wa ishu hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Johari ambapo alipopatikana alisema kuwa, ni kweli alikumbwa na balaa hilo lakini anamshukuru Mungu aliachwa salama licha ya kuibiwa pochi iliyokuwa na vitu mbalimbali.

“Walionifanyia ule mchezo hata siwajui lakini namshukuru Mungu niko vizuri, wamenichukulia pochi yangu iliyokuwa na simu, pesa na vitu vingine, nilienda kutoa taarifa polisi na taratibu za kisheria zinaendelea,” alisema Johari.

Katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi la watu wanaolewesha watu kisha kuwaibia hivyo gazeti hili linawatahadharisha wasomaji wake kuwa makini katika kila eneo wanalokuwa ili kuepukana na majanga kama yaliyomkuta staa huyo