Monday, September 10, 2018

Jack Pemba sasa Kumwaga Pesa Soka la Bongo

Tags

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kwa sasa linahesabu siku chache tu kabla ya kupata dawa ya kupunguza makali ya kuendesha ligi kwa kuingia mkataba wa kimichezo na mfanyabiashara, Jack Marshal Pemba anayeishi Uganda kupitia kampuni yake ya Pemba Sports Africa.

TFF na Jack Pemba wamefikia hatua hiyo ya kuingia mkataba ikiwa ni baada ya pande hizo mbili kufanya mazungumzo wakati viongozi wa TFF walipokutana na mfanyabiashara huyo ambaye anahesabika kama mmoja wa watu wenye fedha nchini Uganda kwenye mchezo baina ya Taifa Stars na Uganda ‘The Cranes’.

Kwa sasa mfanyabiashara huyo amejikita kwenye michezo kwa kudhamini timu kadhaa za soka pamoja na timu nyingine za mpira wa kikapu.

Katika mahojiano maalum aliyofanya mfanyabishara huyo na Spoti Tv nchini Uganda, amesema tayari ameshamalizana na TFF ambao walimuomba kwa ajili ya kuja kuwekeza kwenye soka la Tanzania na muda siyo mrefu atarejea kwa ajili ya kuingia mkataba na shirikisho hilo.Tumekutana na watu wa TFF tangu siku kadhaa hapa Uganda na tumezungumza mambo mengi ambapo wao wameniomba kwa ajili ya kuja kuwekeza kwenye soka la nyumbani kama ambavyo nimekuwa nikifanya huku Uganda.

“Muda siyo mrefu nitarejea nyumbani kwa ajili ya suala hilo la kuingia mkataba na kuanza jukumu hilo la kuwekeza kwenye soka la hapo nyumbani.

“Lakini pia kama mambo yakienda sawa, nitafanya udhamini kwenye moja ya timu za huko kwa sababu sasa mimi ni milionea hasa na ninataka kuja nyumbani kwa ajili ya kuwekeza huko,” alisema Jack Pemba.

JACK PEMBAMimi ni Tajiri Kweli Kweli, JPM Nakuja”