Wednesday, September 12, 2018

Irene Uwoya Azungumzia Ukaribu Wake na Diamond Platnumz

Tags

Msanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya amefunguka mara baada ya Diamond Platnumz kumposti hivi karibuni na kitoandika chochote.

Muingizaji huyo akipiga stori na SnS Tanzania (Simulizi na Sauti) amesema kuwa alichukulia kitu hicho kawaida ingawa watu walitafsiri vibaya.

"Sioni kama ni tatizo kwa sababu aliposti tu picha ambayo mtu mwingine anaweza akaposti. Watanzania wanapenda tu kufikiria vitu, ku-judge wanavyoweza wao, haikuwa tatizo kwangu," amesema Irene Uwoya.

Hapo jana kwenye Biko Jibebe Challenge  Irene Uwoya ndiye alikuwa host wa tukio hilo. Shindano hilo lilianzishwa na Diamond baada ya kutoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Jibebe ambao ameshirikiana na Mbosso na Lava Lava.