Sunday, September 16, 2018

Dharau Zingine Huwa Hazina Faida..Ona Huyu Dada Alivyoadhirika

Tags

Dharau Zingine Huwa Hazina Faida..Ona Huyu Dada Alivyoadhirika
Leo Asubuhi Nikiwa Ubungo bus terminal....
Leo asubuhi nikiwa stand ya mabasi ya ubungo,mdada mmoja wakati anapanda kwenye kagari kake akadondosha simu.Mimi nikamuita ili nimweleze kilichotokea,akanisonya tena msonyo wa dharau sana na nikajuta kumgusa bega kwasababu ya kibao alichonipiga.

Alipoondoa gari nikaiokota hiyo simu na kuondoka zangu,wala sikuizima.

Nafika town simu hiyo ikaita nikapokea kwa shauku ya kujua nani,haya ndo ya kawa maongezi yetu na mpigaji.


Mimi; Hallo habari yako
Yeye; Nzuri
Mimi; nani wewe
Yeye; Mimi ndo mwenye hiyo simu ....
Mimi; Na mimi ndo nilokuita na ukanizaba kibao Pale stand ya ubungo leo na ukanisonya
Yeye; Basi kaka nisamehe naomba unambie ulipo nije tuelewane
Mimi; Nitakwambia baadaye (nikakata simu na kuzima)

Swali nimwambie napatikana wapi au nimpotezee ili liwe fundisho kwake?