Davido Asitisha Ziara Yake ya Muziki Nchini Marekani, Atangaza Kujiunga na Jeshi Nigeria

Davido asitisha ghafla ziara yake ya muziki nchini Marekani, atangaza kujiunga na jeshi Nigeria
Msanii maarufu nchini Nigeria, Davido ametangaza kusitisha ziara yake ya muziki nchini Marekani aliyooita ‘THE LOCKED UP’ na kueleza mashabiki wake kuwa ataungana na jeshi la kujenga taifa la nchi hiyo ili aingie kwenye mafunzo maalumu ya kitaifa ya National Youths Corps Services (NYCS).

Davido kupitia ukurasa wake wa Instagram amewaomba radhi wanaigeria wenzake na kisha kutoa tangazo la kusitisha ziara yake nchini Marekani ili kuungana na wanafunzi waliomaliza vyuo nchini humo kwenye mafunzo hayo maalumu ya kijeshi.Mapema mwezi uliopita Davido alitangaza kuwa ataungana na Jeshi la Kujenga Taifa la nchi hiyo ili kushiriki kwa hiyari kwenye mafunzo yanayotolewa kila mwaka kwa wanafunzi wanaomaliza vyuo nchini humo.

Image may contain: 6 people, people smiling, people sitting

Davido ataungana na wanafunzi waliomaliza vyuo vikuu na vya kati nchini humo, kwenye mafunzo hayo maalumu kwa miezi mitatu Davido atakuwa akifanya mazoezi ya ukakamavu, kulima, kujenga, kufyatua tofali na shughuli nyingine kama ambavyo hapa nyumbani jeshi la JKT wanavyofanya.

Image may contain: 2 people, people standing, sky and outdoor

NYCS ni mpango wa serikali nchini Nigeria wenye lengo la kila mwanafunzi anayemaliza masomo yake ya chuo ni lazima ajiunge na Jeshi la kujenga taifa la nchi hiyo kabla ya kuajiriwa. Inaelezwa kuwa bila ya kupitia kwenye mafunzo hayo ya kijeshi basi hutaweza kuajiriwa serikalini au hata kwenye makampuni binafsi.

Image may contain: 3 people, people sitting and indoor

Hata hivyo, Davido amewatangazia mashabiki wake kuwa atatangaza baadae tarehe rasmi ya kumalizia ziara yake nchini Marekani, baada ya kumaliza mafunzo hayo.