Cardi B Avunja Ukimya, Amjibu Nicki Minaj

Cardi B avunja ukimya, amjibu Nicki Minaj
Kupitia Instagram yake Rapper wa kike Cardi B  kutoka Marekani amjibu Nicki Minaj ambae ndie mpinzani wake mkubwa kwa sasa.

Kabla ya drama hizi kuendelea hawa madada wawili kutoka Marekani walianza vizuri kufanya muziki lakini maigizo yalianza pale waliposhirikishwa katika nyimbo moja na kundi la muziki kutoka nchini humo linalojulikana kama Migos katika nyimbo yao ya Motorsports.

Baada ya maigizo hayo kuendelea Nicki alikuja kuongea katika vyombo vya habari na kudhibitisha kuwa hana ugomvi na Cardi B na kumpongeza kwa mafanikio yake makubwa aliyoyapa kupitia muziki wake,lakini alipoulizwa Cardi B hakuonesha kufurahishwa na maneno hayo ya Nicki.

Baada ya Cardi B kujifungua mtoto wake alianza vibwanga kwani alianza kupost video zinazoonesha akimponda msanii flani ambaye hakuweza kumtaja jina na siku ya maadhimisho ya mitindo yanayofanyika kila wiki katika jiji la New York zinazojulikana kama Harper Bazaar ICONS ambapo ugomvi ulitokea mkubwa hadi Cardi B kumrushia Nicki viatu.

Pia katika mahojiano aliyoyafanya Nicki na kusema “Tukio hilo lilikuwa la udhalilishaji kwa sisi wote wawili,siwezi kuzungumzia malezi ya mtu inanishangaza jinsi watu wanavyopenda kunifanya mimi ndio nionekane mbaya mmeona ile video iliyovuja lakini mimi ntaonekana mpumbavu”

Nicki aliongeza ” Mwanamke huwezi kumuachia mwanaume kama mwenyewe hataki,una hasira na nani ? aliuliza Nicki Umenikuta kwenye muziki sijawahi kutembea na DJ ili wapige ngoma zangu”

Baada ya mahojiano hayo ya Nicki kuhusu kumzungumzia Cardi B kuwa amewahi kutembea na DJ ili apigiwe ngoma zake hivyo Cardi B anabebwa basi Cardi wiki hii na yeye kaamsha mambo baada ya kujibu mapigo kwa kupost orodha ya wasanii waliouza albam zao kwa wingi zaidi mwaka 2018 huku katika orodha hiyo hakuiweka albam ya Nicki Minaj ya ‘Invasion Of Privacy’ na queen ” huku akiandika chini ya post hiyo kuwa ” Number dont fuckin lie” yaani Namba haidanganyi.
MaoniMaoni Yako