Bifu la Pogba na Mourinho Lafufuka Tena!

KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba amelifufua tena bifu lake na kocha Jose Mourinho baada ya kuwaambia kuwa uhusiano wao haupo vizuri.

Katika mahojiano aliyofanya juzi, Pogba alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa hawezi kujiapiza kuwa atadumu kwa muda mrefu katika Klabu ya Manchester United.

Katika siku za karibuni, kumekuwa na taarifa kuwa wakala Mino Raiola amekuwa anahaha kumta-futia timu Pogba na kuna muda alikutana na uongozi wa Real Madrid.
 
➤:AJIRA MPYA BOFYA LINKI HII:
Pogba amekuwa haelewani na kocha wake, Mourinho tangu msimu uliopita, ambapo mara kadhaa aliwekwa benchi na inasemekana hivi karibuni walirushiana maneno makali.

Kauli za Pogba bila shaka zitafungua milango kwa klabu mbalimbali kuanza kumfukuzia kiungo huyo.

Pogba alisema hawako sawa na Mourinho kutokana na ukweli kuwa kila mmoja ni kama hana imani na mwenzake.

Alipoulizwa kama yupo tayari kuondoka katika klabu hiyo, Pogba alijibu hawezi kujiapiza kuwa miaka yote atadumu katika timu hiyo.

Klabu ambazo zinatajwa kumtaka Pogba ni pamoja na Barcelona na timu yake ya zamani Juventus.

MaoniMaoni Yako