Azam wavamia Mwadui, Kutinyu kimeeleweka

Dar es Salaam. Klabu ya Azam FC tayari imewasili mkoani Shinyanga kwa ajili ya
mchezo wao dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa Ijumaa katika uwanja wa Mwadui Complex.
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd, amesema kikosi chao kipo vizuri kuelekea mchezo
huo na wanachohitaji ni ushindi kwa namna yoyote.
“Wana uwanja mzuri na tunapokuwa katika viwanja kama hivi huwa tunatafuta ushindi wa
namna yoyote, kwa hiyo tunaamini kwamba tutatoka na pointi tatu tukiwa hapa,”
alisema Jaffer.
Akizungumzia wachezaji wao waliokuwa na timu ya Taifa Stars, Jaffer amesema 
wamerejea wote kasoro Tafadzwa Kutinyu ambaye alikuwa pembezoni mwa Afrika lakini
naye anatarajiwa kuingia kesho.
“Wachezaji waliokuwa na timu za taifa wamerejea lakini Kutinyu yeye ataingia Dar es
Salaam kesho Alhamisi na moja kwa moja ataunganisha ndege mpaka Mwanza halafu
atakuja kujiunga na timu huku Shinyanga,” alisema.

Nafasi za kazi mpya zilizotangazwa leo Jumatano 12 September 2018- Apply Now