Amber Lulu Atamani Kujiunga lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Msanii wa muziki Bongo, Amber Lulu amesema kuwa anatamani siku moja awepo kwenye lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Muimbaji huyo kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema kuwa  anaona lebo hiyo ina msanii mmoja tu wa kike hivyo si vibaya na yeye kuwepo hapo kama msanii wa pili wa kike.

"Nilikuwa naona WCB wana msanii wa kike tu mmoja, Queen Darleen nikaona kwanini mbona watu tu wengi tupo tunaangaika kila siku wakati watu wanasaini. Mimi mwenyewe nahitaji nafasi, yale mandinga yananichanganya kinoma," amesema Amber Lulu," amesema.

Alipoulizwa iwapo amewahi kukutana na Diamond na kuzungumzia hilo, Amber alijibu, 'Hapana kwa sababu mimi na yeye tunaonana muda mfupi kwenye party na nini, so sijapata time ya kuongea naye.'.