Wolper Aibua Mapya, Adai Harmonize Bado Anampenda

Msanii wa filamu, Bongo Jacqueline Wolper ametaja sababu zilizopelekea ex-boyfriend wake, Harmozie kutaja orodha wa wanaume 11 ambao alidai waliwahi kutoka kimapenzi na mrembo huyo.

Muigizaji huyo akizungumza akiwa nchini Kenya na Kiss FM amesema kuwa kilichopelekea Harmonize kufanya hivyo ni maumivu ya mapenzi.

“Binafsi sikuchukia wala sikukasirika kwa sababu niliona amepaniki, you know a guy love me a lot, kwa hiyo niliona amepaniki tu na ni maumivu ya mapenzi na sikumshangaa,” amesema Wolper.

Utakumbuka usiku wa kuamkia May 8, 2018 ndipo Harmonize alitoa orodha hiyo, ni baada ya Wolper kwenye moja ya interview kudai kuwa mpenzi wa Harmonize wa sasa, Sarah ni mlezi wa wana.