Monday, June 11, 2018

Wahukumiwa Miaka 15 Jela kwa Kesi ya Uhujumu Uchumi

 


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 15 jela Joephat Joseph Mushi(mfanyabiashara ya samaki) na Said Omary Sisige (Dereva wa roli) na kuwaachia huru washitakiwa saba katika kesi ya uhujumu uchumi namba 2/2017.


Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mawakili wandamizi Saraji Iboru na Paul Kimweri ambapo mshitakiwa wa kwanza alikuwa akitetewa na jopo la Mawakili wanne Victor Mkumbe, Simon Mwakolo, Habib Kamru na Jackson Ngonyani ambapo mshitakiwa wa pili alikiwa akijitetea mwenyewe.

Walioachiwa huru na Hakimu Michael Mteite ni Agripa Benjamin, Pius Jacob Joseph, Said Swedi, Shaban Sankwa, Lugano Francis Mwakapala, Ibrahim Miller na Andrew Kachengo.

Akisoma hukumu  hiyo Hakimu Mteite amesema Mahakama inawatia hatiani mshitakiwa wa kwanza Josephat Mushi na Said Omary katika makosa saba kosa la kwanza ni kula njama, kosa la pili kughushi, kosa la tatu kutoa maelezo ya uongo, kosa la nne kuondoa lakiri, kosa la tano kumiliki mali isiyolipiwa ushuru, kosa la sita kughushi nyaraka na kosa la saba kuitia hasara wizara ya uvuvi.

Hakimu Mteite amesema adhabu zote zitakwenda kwa pamoja hivyo watatumikia kifungo cha miaka kumi na tano jela na kulipa fedha kama zilivyoainisha.

Aidha Mteite ameamuru kuteketezwa shehena yote ya samaki kutokana na kukaa muda mrefu na kuzingatia afya ya binadamu ambayo ni muhimu kuliko mali.

No comments:
Write comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Facebook