Monday, June 11, 2018

Viongozi wa dini msiwe na wasemaji ambao sio viongozi – Rais Magufuli (+video)

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaomba viongozi wa dini zote kutokuwa na wasemaji ambao si viongozi wa dini.

Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli amewasihi viongozi wa dini kujiepusha kuwatumia watu wasio viongozi wa dini kuzungumzia masuala ya dini, na kubainisha kuwa kufanya hivyo ni kuleta mkanganyiko.
"Msiwe na wasemaji ambao sio viongozi wa dini, mnapokuwa viongozi wa dini halafu mnawatumia wasemaji ambao sio viongozi wa dini labda wanasiasa, mtakuwa mnachanganya dini na siasa ambacho ni kitu kibaya sana''.Alisema Magufuli
Kwa hiyo panapozungumzwa jambo lolote linalohusu dini lizungumzwe na viongozi wa dini wenyewe, kama ni Masheikh wazungumze Masheikh, kama ni Mufti azungumze Mufti, kama ni Askofu azungumze Askofu, kama ni Padre azungumze Padre, kama ni Mchungaji azungumze Mchungaji, msitafute wasemaji wengine kwa niaba yenu" amesisitiza Rais Magufuli
Magufuli alikuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti uliopo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco.
Ujenzi wa msikiti huo utakamilika mwezi Aprili 2019.

Ujenzi wa msikiti huo umepangwa kukamilika mwezi Aprili 2019, na katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Abdelilah Benryane na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally.
Akizungumza katika eneo la ujenzi Rais Magufuli amemtaka Balozi Benryane kufikisha shukrani zake za dhati kwa Mfalme wa Morocco kwa kutekeleza ahadi hiyo ambayo ameielezea kuwa ni muhimu kwa kuwa imelenga kuimarisha mazingira ya kuabudia.
"Naomba unifikishie shukrani zangu kwa Mfalme Mohamed VI kwa kutekeleza ahadi hii, nimefurahishwa sana na maendeleo ya ujenzi huu, pia tunamshukuru kwa kutujengea uwanja wa mpira katika Makao Makuu Dodoma, tunaamini uwanja huu pia utajengwa na utasaidia kuinua michezo nchini mwetu" amesema Mhe. Rais Magufuli.
Msikiti unaojengwa utakuwa na uwezo wa kuchukua waumini 6,000 hadi 8,000 kwa mara moja na utakuwa ndio msikiti mkubwa kuliko yote Afrika Mashariki na Kati.

by richard@spoti.co.tz

 

No comments:
Write comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Facebook