Vincent Barnabas atangaza kustaafu soka


Arusha. Winga Vincent Barnabas baada ya kuiongoza Mtibwa Sugar kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam ametangaza kustaafu soka.
Akizungumza wakati akikabidhiwa tuzo ndogo ya shukrani na Mkurugenzi wa Mtibwa Sugar, Barnabas amesema ameamua kustaafu kucheza soka baada ya kuona umri wake umeenda na anatamani kuambukiza kipaji chake kwa vijana chipukizi.
"Nimechezea Mtibwa Sugar kwa miaka nane mfululizo na nilianzia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na mechi hii ya fainali ya FA dhidi ya Singida ndio mchezo wangu wa miwsho kucheza," alisema Barnabas na kuongeza
'Hata hivyo sitabaki na kipaji changu bali nitakuwa kocha muda si mrefu namalizia kozi yangu ya ukocha ili na mimi nifundishe vijana mpira maana tayari nina uzoefu wa kutosha."
Akimkabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi wa Mtibwa, Jamal Bayser alisema kwa miaka nane mfululizo Barnabas aliyochezea Mtibwa amekuwa na nidhamu ya hali ya juu huku akicheza kwa uzalendo hivyo hawawezi kumuacha aondoke.
"Amefanya makubwa katika klabu yetu hivyo aliposema azma yake ya kustaafu tumemuanzishia kozi fupi ya ukocha na muda wowote  akimaliza tutamkabidhi timu ya vijana chini ya miaka 20 kuwa kocha hii yote kutambua mchango wake.
MaoniMaoni Yako