VIDEO: Siku za Mfaransa ndani ya Simba zahesabika


Nakuru. Siku za kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre zinahesabika ndani ya klabu hiyo baada ya kubainika kuwa amebakisha wiki mbili tu kabla ya kumaliza mkataba wake na timu hiyo.
Lechantre alijiunga na Simba Januari 18 mwaka huu hivyo mkataba wake unafikia tamati Juni 18.
Afisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema watafanya tathmini baada ya mkataba huo kumalizika na kuzungumza na Lechantre juu ya uwezekano wa kumpatia kandarasi mpya.
"Mkataba wa Lechantre unamalizika tarehe 18, baada ya hapo tutazungumza kuona kama ataendelea kuwa nasi," alisema Manara.
"Niwaombe mashabiki waendelee kuwa na uvumilivu. Kocha ametupa ubingwa hivyo kufanya vizuri kwenye mechi moja ama mbili isiwe sababu ya kutoa lawama nyingi, wawe na subira," aliongeza Manara.