Friday, June 8, 2018

VIDEO: Dr shika amtambulisha msanii wake asema atafunika wasanii wote

 

Dk. Shika leo, Juni 8, 2018 katika Mkutano wake na Waandishi wa habari amemtambulisha Msanii wake mpya atakaye kuwa anamsimamia katika zake za muziki aitwaye Godson ambaye pia ametambulisha nyimbo yake mpya iitwayo ‘Relax’.

Dk. Shika katika Mkutano wake huo amesema kwa msanii yoyote atakayetaka kusimamiwa na yeye yupo tayari lakini anaanza na huyo aliyemtambulisha kwa siku ya leo.
“Nina uhakika kwamba atafunika wasanii wengi , kwahiyo jaribuni kumfuatilia,” amesema Dk. Shika.
Dk. Shika ni daktari wa magonjwa ya binadamu, aliyejipatia umaarufu miezi kadhaa iliyopita kupitia kufika dau wakati wa mnada wa Majumba ya Lugumi

No comments:
Write comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Facebook