Tetesi za soka Ulaya 01.06.2018

Kocha wa Real Madrid anayeondoka Zinedine Zidane na Mshambuliaji Gareth BaleChelsea itajaribu kumshawishi Zidane kuwa mkufunzi wake mpya . (sun)
Matumaini ya klabu ya Manchester United ya kumsajili Gareth Bale, 28, huenda yakafifia huku mchezaji huyo wa taifa la Wales akitarajiwa kusalia kufuatia kuondoka kwa Zidane. (Daily Mirror)
Real Madrid huenda ikamnyatia mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino - ambaye alitia saini mkataba mpya wa miaka mitano na timu yake wiki iliopita- ili kuchukua mahala pake Zinedine Zidane aliyeondoka. (Daily Mirror)
Lakini Real pia inamtaka kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, amaye aliiongoza The Reds kufika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya. (Sun)
Kandarasi ya Pochettino katika klabu ya Spurs haina kipengee ambacho kinaweza kumruhusu kuondoka na mwenyekiti wake Daniel Levy yuko tayari kuhakikisha kuwa anasalia katika klabu hiyo.(Daily Telegraph)
Napoli Maurizio Sarri
The Blues pia huenda wakamlenga mkufunzi wa Ufaransa na Paris St-Germain Laurent Blanc kuchukua mahala pake Antonio Conte. (Daily Mail)
Chelsea inasema kuwa haitalipa dau la £7m ili kununua kandarasi ya mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri. (Guardian)
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich angependelea kulipwa kitita cha £1.17bn iwapo ataamua kuiuza Chelsea (Times)
Chelsea imesitisha mazungumzo ya kandarasi mpya na kipa wake Thibaut Courtois na huenda wakamuuza raia huo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26. The Blues inalenga kumsajili kipa wa Roma na Brazil Alisson, 25. (Sky Sports)
Gonzalo Higuain
Juventus imeiuliza Chelsea iwapo inamhitaji mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 30, ikiwa ni katika mipango ya kumsajili tena mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 25. (London Evening Standard)
Kocha mpya wa Arsenal Unai Emery anataka kumnunua kiungo wa kati kinda Yacine Adli 17 kutoka Paris St-Germain.
Unai Emery
Mchezaji huyo anayeichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 pia amevutia timu kama vile Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid. (London Evening Standard)
Newcastle imehusishwa na beki wa klabu ya Sassuolo 26 Gian Marco Ferrari, ambaye alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Sampdoria. (Newcastle Chronicle)
Peter Schmeichel, 54
Kipa wa zamani wa Manchester United Peter Schmeichel, 54, anakaribia kujiunga na klabu ya Sporting kama mkufunzi wa kipa. (Correio da Manha, via Sport Witness)
Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Spurs Harry Redknapp anaamini kwamba mpwa wake , Frank Lampard, anafaa kumsajili nahodha wa zamani wa Chelsea Jhn Terry, 37, katika klabu ya Derby. (Talksport)
Harry Redknapp
Manchester United inatafuta kumsajili afisa wa kusaka wachezaji nchini Ufaransa huku Klabu hiyo ikiendelea kuimarisha mtandao wake wa utafutaji wa wachezaji wenye vipawa . (Manchester Evening News)
MaoniMaoni Yako