Siri Gari Mpya ya Diamond Yafichuka


DAR ES SALAAM: Lile gari jipya la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aina ya Land Cruiser, ambalo limedaiwa ni toleo jipya la 2018 kuzua gumzo mitandaoni, siri imefichuka kuwa si jipya bali ni la zamani lakini limebadilishwa muundo na Kampuni ya TTTR Auto Up Grades. Co. Ltd iliyopo Mikocheni B jijini Dar.

Chanzo makini kililieleza Amani kuwa tangu awali mzazi mwenziye na mwanamuziki huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ alipoanika ndinga lake jipya ilionekana wazi kwamba msanii huyo aliamua kulipiza kisasi kwa kutupia Land Cruiser hilo.

Diamond kwa mara ya kwanza alianika gari hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo watu wengi walikuwa wakimpongeza kwa hatua hiyo ya kununua gari hilo jipya la mwaka 2018.

SIRI YAFICHUKA

Baada ya Diamond kuanika gari hilo, Amani lilidodosa mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyomtengenezea gari hilo ambaye alikiri kuwa ni la zamani lakini wamelifanyia matengenezo na kuonekana jipya huku akigoma kutaja gharama yake.


“Sisi ndiyo tumelitengeneza hilo gari na kulibadilisha kama kutoka katika gari la zamani lakini hatuna mamlaka ya kusema ni kiasi gani mteja wetu katumia kwenye matengenezo hayo mpaka mwenyewe aruhusu,” alisema mmiliki huyo aliyeomba hifadhi ya jina.


Kumekuwa na ushindani mkubwa kati ya timu Zari na timu Diamond baada ya msanii huyo kulionyesha gari hilo kwa mara ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii na kuzua mjadala huku kila mtu akimsifia mtu wake.
MaoniMaoni Yako