Simba Walivyoishuhudia Kakamega Ikiimega Yanga Kwa Mabao 3-1 Kenya

Wachezaji wa kikosi cha Simba wakiongozwa na Kocha Msaidizi wa timu, Masoud Djuma, leo walikuwa Uwanjani kuishuhudia Yanga ikicheza dhidi ya Kakamega Boys.


Katika mchezo huo ambao Yanga imekubali kufungwa mabao 3-1 na kuondolewa kwenye mashindano hayo ya SportPesa Super CUP, Simba walipata nafasi ya kuutazama mchezo huo ili kuzisoma timu zote mbili.

Simba watashuka dimbani kesho Jumatatu kucheza dhidi ya Kariobang Sharks, mchezo ukianza majira ya saa 9 alasiri.

Wakati huo wachezaji Shiza Kichuya na Mohamed Rashid wameondoka pamoja leo kuelekea Nakuru ili kujiunga na kikosi cha Simba kwa ajili ya mashindano hayo.