Sasha 'Nitaendelea Kupiga Picha za Nusu Utupu Baada ya Kupumzika Kwa Muda'


LICHA ya Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kuwafungia na kuwaita na kuwakanya wasanii ambao wamekuwa wakijianika nusu utupu, muuza nyago kwenye video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Sasha Kassim amefunguka kuendelea kupiga picha za nusu utupu.

Akizungumza na Gazeti la Amani, Sasha alisema kuwa anajiandaa kupiga picha nyingine ambazo kama ni nguo za ndani zitaonekana nadhifu na zenye kuvutia na pia zitapungua ‘ukali’.

 “Nilipotea kwa sababu niliibiwa akaunti yangu ya Instagram, si unajua ilikuwa na picha nyingi sana ila sasa hivi najiandaa kupiga picha nyingine mpya zitakuwa zikinionyesha sehemu zangu za mwili lakini zitakuwa zenye kujistiri kidogo,” alisema Sasha

MaoniMaoni Yako