NSAJIGWA FUSO NAE AACHANA RASMI NA YANGA


-Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Shadrack Nsajigwa Fuso ameondoka rasmi ndani ya Klabu ya Yanga Sc baada ya mkataba wake kuisha. Nsajingwa hakuambatana na klabu hiyo Kenya kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup.

-Yanga ambayo imetolewa huko Kenya na timu ya Kakamega Home Boys imepanga kutomuongezea mkataba na kuachana naye pamoja na Noel Mwandila ambaye naye mkataba wake unaisha mwisho wa mwezi huu. Nsajigwa amekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Yanga kwa msimu mmoja baada kurithi mikoba ya Juma Mwambusi aliyeondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kuisha pia.

-Rafiki wa karibu wa Shadrack Nsajigwa Fuso amesema ni kweli kocha Nsajigwa ameachana rasmi na klabu hiyo kwani amekuwa akifanya kazi bila mkataba wowote baada ya mkataba wake kuisha March mwaka huu pia kocha huyo hajalipwa mishahara kwa miezi minne mara ya mwisho kwa kocha huyo kupokea mshahara ni mwezi January, sababu nyingine ni kocha huyo kuandamwa na mashabiki wa klabu hiyo ajiuzulu kutokana na matokeo mabaya kwa klabu ya Yanga..

-Yanga ambayo itawasili leo kutokea Kenya imefanya mazungumzo na kocha Fred Minziro kurithi mikoba ya Shadrack Nsajigwa ndani ya klabu hiyo. Minziro alikuwa kocha wa KMC ila kwa sasa hana maelewano na klabu hiyo baada ya kuambiwa atapangiwa kazi nyingine na nafasi ya kocha mkuu kupewa Ettiene Ndayiragije.

@yossima Sitta Jr.