Saturday, June 9, 2018

Ngoma nje wiki tisa azam

 


-Klabu ya Azam Fc kupitia kwa Daktari wa timu hiyo Mwanandi Mwankemwa imesema mshambuliaji wao mpya  Donald Ngoma atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tisa.

-Ngoma ambaye alikuwa mchezaji wa Yanga alisajiliwa na Azam kwa mkataba wa mwaka mmoja na kupelekwa Afrika Kusini Katika hospitali ya St. Vincent Parrot kufanyiwa vipimo kujua ukubwa wa jereha lake.

-Mwankemwa amesema Ngoma alikuwa ana uvimbe kwenye goti la kulia ambapo baada ya vipimo imeonekana alikuwa amechanika kidogo japo tayari ameanza kupona.

-Pia Docta Mwankemwa amesema Ngoma hatafanyiwa upasuaji badala yake ataendelea kufanya mazoezi mepesi ya kawaida mwenyewe kabla ya kupona kabisa na kurejea uwanjani.

-Kwa maana hiyo mchezaji huyo atarejea uwanjani mwezi wa nane (August) na sasa atayakosa mashindano ya Kagame Cup ila atakuwa fiti kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara (vpl) 2018/19.
@yossima Sitta Jr.

No comments:
Write comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Facebook