Ndemla ahusishwa kutua yanga

Wakati taarifa zikielezwa kuwa Simba wapo kwenye mazungumzo na kiungo wake, Said Ndemla ili kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea, watani zao wa jadi wanahusishwa kutaka saini ya mchezaji huyo.

Ndemla hajawa sehemu ya kikosi cha kwanza katika msimu wa 2017/18 na badala yake alikuwa akianzia benchi kwa takribani mechi zote ambazo wekundu hao wa Msimbazi wamecheza msimu uliomalizika.

Taarifa zinaelezwa kuwa Yanga wameanza mazungumzo naye kwa ajili ya kumsajili ili kwenda kuboresha safu yao ya kiungo ambayo haifanyi vema kwa sasa.

Taarifa zinasema kuwa Ndemla ameshamaliza mkataba ndani ya Simba lakini vilevile inaelezwa kuwa uongozi wa klabu yake umeanza mazungumzo naye kwa ajili ya kuongeza mwingine.

Endapo Ndemla atajiunga na Yanga atakuwa anaungana na aliyekuwa mchezaji mwenzake, Ibrahim Ajibu aliyeondoka Simba kabla ya msimwa 2017/18 kuanza