NBA: Golden State Warriors yainyuka Cleverland, LeBron James ambwaga Stephen Curry

Timu ya kikapu ya Golden State Warriors kutoka kanda ya Magharibi imefanikiwa kushinda katika mchezo wa fainali ya kwanza ya NBA dhidi ya Cleveland Cavaliers katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia Ijumaa hii katika uwanja wa Oracle Arena, California.

Katika mchezo huo Golden wameshinda kwa jumla ya vikapu 124 dhidi ya 114 vya Cleverland.
LeBron James alikuwa nyota wa mchezo huo kwa upande Cavaliers baada ya kushinda jumla ya vikapu 51 wakati kwa upande wa Worriors, Stephen Curry akiongoza kwa kutupia vikapu 26 akifuatiwa na Kevin Durant aliweka vikapu 26.
Timu hizo zitakutana tena siku ya Jumapili katika mchezo wa fainali ya pili.

by richard@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako