Tetesi Za Soka Barani Ulaya leo Juma pili 03/06/2018

Mshambuliaji Gareth Bale ataendelea kuwafanya Manchester United kusubiri uamuzi kuhusu mustakabali wake mpaka pale atakapoona nani atakayekuwa meneja mpya wa Real Madrid. (Express)
Kiungo wa Croatia anayewaniwa na Manchester United Mateo Kovacic amegusia kuhama timu ya Real Madrid akisema anahitaji muda wa kucheza zaidi.Ameanza michezo 10 tu ya La Liga msimu uliopita.(Sun)
Cristiano Ronaldo aliwambia wachezaji wenzake kabla ya fainali ya ligi ya mabingwa kuwa alitaka kuihama klabu ya Real Madrid.Kuna tetesi kuwa Ronaldo ana mpango wa kurejea Manchester United. (Marca)
Wakati huohuo Real Madrid imeondoa matumaini yao kwa Meneja wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino baada ya kutaka awe mbadala wa Zinedine Zidane aliyeondoja juma lililopita.(Sky Sports)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amekuwa pendekezo jipya la Real Madrid na amekuwa akipendwa na mashabiki wa timu hiyo ya Uhispania. (Express)
Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini ataka kumsajili kiungo Jack Wilshere kama ataondoka Arsenal. (Star)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameweka kipaumbele kumnyakua Marco Verratti, 25, wa Paris St-Germain.(Mirror)
Meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique huenda akawa Meneja mpya wa Chelsea baada ya kuanza tena mazungumzo na the Blues. (Sport)
Meneja wa Arsenal Unai Emery anataka kufanya usajili wake wa kwanza kwa kiungo wa kati wa Sevilla,Steven N'Zonzi.
Pia Arsenal inamtolea macho winga Gelson Martins.Mreno huyo alifunga magoli 13 msimu uliopita.(O Jogo - via Football.London)
Meneja mpya wa Everton Marco Silva anataka kumsajili mshambuliaji wa West Ham Marko Arnautovic, 29, lakini Manchester United pia imekuwa ikivutiwa na mchezaji huyo.(Sun)
Kiungo wa Stoke City Badou Ndiaye ataondoka Potters kipindi cha majira ya joto, wakala wake amethibitisha.Mchezaji huyo mwenye asili ya Senegal amekuwa akihusishwa na timu ya Wolves. (Birmingham Mail)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amethibitisha angependa kujaribu kuwa kocha wa timu ya taifa miaka ya mbeleni. (Manchester Evening News)
Watford inasema haitakubali kumuuza kiungo wake mshambuliaji Richarlison,21 kwa ada pungufu ya Paundi Milioni 40 na hawatamuuza mbazili huyo kwenda Everton kwa gharama yoyote ile.(Mirror)
Brighton wanatamani bado kumsaini Paddy McNair wa Sunderland baada ya dau la Paundi Milioni 2 kukataliwa.(Argus)
Meneja mpya wa Derby Frank Lampard amesema anataka kuwa meneja wa timu ya taifa ya England siku za usoni. (Sun)