Mrithi wa jezi namba 11 kapatikana bado namba 8 ya Niyonzima

Msimu uliomalizika jezi namba nane ilikuwa ikivaliwa na kiungo chipukizi Maka Edward ambaye tayari amesema hataendelea kuitumia jezi hiyo kwa 'heshima' ya mchezaji mpya anayekuja Yanga.

Sasa Afisa Habari wa Yanga Disman Ten kama kawaida yake tayari amewaweka mkao wa kula mashabiki wa timu hiyo kupokea ujio wa mchezaji atakayetumia jezi hiyo.

Namba 11 tayari imeshapata mvaaji, Marcelin Koukpo mshambuliaji wa Kimataifa wa Benin aliyetua jana usiku na kusaini mkataba wa miaka 2.

Huyu amerithi mikoba ya Donald Ngoma aliyetimkia Azam FC.

Naona mji umeanza kutulia sasa......!
MaoniMaoni Yako