"Sina mpenzi ila uyu ndio shemeji yenu": Rosa ree


Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Rosa Ree amefunguka kuhusu maisha yake ya kimapenzi.

Rapper huyo amesema kwa sasa yupo single ila atakapoingia katika mahusiano hatosita kuwajuza mashabiki wake.

“Niko na only my hustle, am marry with my hustle guys, ni kitu ambacho nasema sana sina mpenzi lakini kweli na siku nikiwa na mpenzi mtamfahamu na nitawaambia huyo ndiye shemeji yenu, yeah!, let just wait for that day,” Rosa Ree ameiambia Bongo5.

Alipoulizwa baada ya kukabidhiwa mjengo na menejimenti yake mpya, Dimo production ataishi na nani, alijibu; ‘Yes, mimi mwenyewe na familia yangu watakuwepo around me lakini for now is just me’.

Rosa Ree kwa sasa anatamba na ngoma ‘Way Up’ ambayo amemshirikisha rapper Emtee kutoka Afrika Kusini, video ya wimbo huo inatarajiwa kutoka leo, June 01, 2018.

MaoniMaoni Yako