Matibabu ya Wema Sepetu India, Mimba Yatajwa


DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya mrembo Wema Sepetu kudaiwa kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu, habari nyuma ya pazia zimeleza kuwa, sehemu kubwa ya tatizo linalomsumbua mrembo huyo ni kusaka ujauzito.

 Mei 29, mwaka huu, Wema alishindwa kutokea katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar katika kesi ya madawa ya kulevya inayomkali ambapo mama yake aliwasilisha nyaraka zilizoonesha kuwa bintiye amekwenda nchini India kwa ajili ya matibabu.

 Chanzo kilicho karibu na mrembo huyo kimeeleza kuwa, kwa muda mrefu Wema amekuwa akihangaika kupata mtoto hivyo ameona aende India ili kuweza kusaka suluhu.

“Wema anatamani kuwa mama jamani, hajachoka na ha hakati tamaa. Ameamua kwenda India na nasikia matibabu ya safari hii nasikia yatahusisha pia upasuaji,” alisema mtoa habari huyo.

 Baada ya kunasa ubuyu huo, Ijumaa lilijaribu kuwasiliana na mama yake mzazi Wema, Miriam Sepetu bila mafanikio lakini hata hivyo, baadaye alipatikana meneja wake, Neema Ndepanya, akafunguka:

“Mimi ninachofahamu ni kwamba amekwenda India kwa ajili ya matibabu ya tumbo na si vinginevyo,” alisema Neema. 
MaoniMaoni Yako