Manara: "Naogopa kumtelekeza mke wangu"

Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Mabingwa wa Ligi Kuu (VPL) Simba SC, Haji Manara amesema anauchukia umasikini kwa kiwango cha juu ila hapendi kuwa tajiri kwa madai anahofia kutomkumbuka Mungu wake pamoja na kumtelekeza mke wake ambaye anampenda kwa dhati.

Kauli hiyo ya Haji Manara imekuwa yenye mtazamo tofauti na vijana wengi wa kizazi cha sasa ambao wao wanaamini katika ndoto zao ili mtu aweze kuwa na maisha mazuri ni lazima awe tajiri mwenye kumiliki vitu vingi vyenye thamani ya juu.

"Mimi sipendi kuwa tajiri yaani sipendi kabisa. Ninapenda kuwa katika maisha ya hivi hivi kawaida maana nikibadilika naona kama ni mateso tu. Naiona hiyo fursa na watu wengi wananiambia niutumie umaarufu ili niwe tajiri lakini kiukweli naogopa", amesema Manara.

Pamoja na hayo, Manara ameendelea kwa kusema "ninachoogopa kuwa tajiri muda mwingine utajiri unampa mtu kibri 'ujeuri', kutomjua Mungu hata kudharau watu sasa mimi naogopa kwanini nipate mitihani ya namna hiyo. Utajiri unaweza kutongozwa na hata na mtu usiyemtarajia, atakuja mwanamke atajifanya anakupenda kumbe anataka pesa tu, mimi sitaki nampenda mke wangu".

Kwa upande mwingine, Haji Manara amesema yeye kikubwa anachohitaji ni kupata pesa za kula, kusomesha watoto na kupata tiba sahihi lakini sio jambo la kuwa tajiri