Sunday, June 3, 2018

Mambo Mswano, Simba Yamalizana Na Muzamiru, Yamuongezea Mkataba

 

Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba wamemalizana na kiungo wao Muzamiru Yassin ambaye alitaka kuona mambo yake yanakaa sawa kabla ya kuungana na kikosi jijini Nairobi.

Simba ipo mjini Nakuru kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajia kuanza leo mjini Nakuru.


Muzamiru amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Simba na leo anatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam kwenda Nakuru kuungana na kikosi.


Kabla yake, Simba ilimalizana na Shiza Kichuya ambaye alikuwa amepata ofa kadhaa za kucheza nje ya Tanzania na alikuwa tayari kuondoka.

No comments:
Write comments

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Facebook